Edit

wikiHow:Swahili language project/About wikiHow

EditUmuhimu wetu

Fikiria juu ya ulimwengu ambao mtu yeyote anaweza kujifunza namna ya kufanya chochote kwa urahisi zaidi. Ulimwengu ambao mabilioni ya watu wanaboresha maisha yao, kwa njia za kawaida na za kipekee,kutokana na fursa ya kutumia maelezo mapana ya hatua kwa hatua katika lugha nyingi. Huo ndio ulimwengu tunaotaka kuuanzisha.WikiHow, ni jamii ya watu walio tayari kujitolea kushirikishana,kupanga, kuanzisha au kuboresha taarifa kwa lengo la kuwasaidia wengine.[1] Mapenzi ya pamoja ya kuanzisha mkusanyiko bora wa mwongozo wa namna ya kufanya jambo ndio msukumo wetu. Tunaboresha kila makala mpaka pale tunapodhani imekuwa makala moja yenye msaada zaidi wa maelekezo juu ya mada husika yapatikanayo popote.


Tukitambua kuwa lengo hili kuu tamaniwa litachukua miaka kulifanikisha, tunafurahia kujua kuwa tayari kila siku tumekwishasaidia mamilioni ya watu.EditTunachokifanya

WikiHow ni juhudi za pamoja katika kuanzisha miongozo yenye msaada zaidi ulimwenguni juu ya namna ya kufanya jambo. Kama Wikipedia, WikiHow inatoa fursa kwa mtu yeyote kuandika au kuhariri kurasa katika tovuti. Maelfu ya watu ulimwenguni kote wameshirikiana kuandika makala za namna ya kufanya jambo fulani. uchambuzi wa Google unaonesha kuwa, Kwa mwezi, zaidi ya watu milioni 40 wanasoma WikiHow na Quantcast wametupa daraja la 150 miongoni mwa tovuti maarufu sana.


WikiHow kwa sasa ipo kwa lugha ya kiingereza, kispaniola, Kireno, KiJerumani, Kifaransa, Kiitaliano, and Kidutch. Matumani yetu mwishowe tuzindue WikiHow katika lugha nyingine nyingi zaidi.

EditSisi ni kina nani?

Kiini cha wikiHow kinaundwa na jamii ya kusisimua ya waandishi na wahariri wa kujitolea kutoka katika nchi nyingi ulimwenguni. Kila anayeshiriki/ kuchangia wikiHow, anafanya hivyo kwa sababu ni jambo kufurahisha. Sababu nyingine zinazowafanya watu kushiriki ni pamoja na shauku ya kuwasaidia wengine, furaha ya kufanya jambo kubwa kwa ushirikiano ambapo mtu peke yake asingeweza kulifanikisha, msisimko wa kuwa unasomwa na hadhira kubwa sana, na tamaa ya kujenga ujuzi hasa kama vile uandishi na uongozi.


Waandilishi wa wikiHOw,Jack Herrick na wafanyakazi wachache wikiHow:waajiriwa wanaosaidia kusukuma gurudumu hili la wikiHow. Makao yetu makuu yapo ndani ya nyumba, downtown Palo Alto,California.

EditWikiHow inavyofanya kazi

Maudhui yetu hubadilika kila siku kwa sababu wikiHow huhaririwa na mtu yeyote. Kila badiliko lililofanyika kuweza kuonekana katika orodha ya Mabadiliko ya hivi karibuni, ambayo hupitiwa mara kwa mara. Mabadiliko dhaifu huondolewa haraka sana na wafanya doria wakujitilea kulinda mabadiliko mapya yanayofanyika. vyombo vingine kadhaa vya kuthibiti ubora hufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa kila makala inaendelea kuwa nzuri zaidi na zaidi, kulingana na watu wengi zaidi kuchangia ujuzi na maarifa yao ya kipekee.


Kupitia leseni ya Creative Commons, inayoruhusu wikiHows'kuchapishwa tena na shirika lolote au mtu yeyote kwa dhumuni lisilo la kibiashara, tunagawa maelekezo yetu bila gharama. pia, tunagawa vyanzo vyetu vya programu vilizo wazi bila gharama.


Sisi tu shirika chotara, kampuni kwa ajili ya faida iliyolenga kuanzisha bidhaa kwa ajili ya umma wa kimataifa kulingana na utume wetu Utume. Tunajiwezesha wenyewe kifedha kwa kuonyesha matangazo hiari. Tunaruhusu mtu yeyote kuficha matangazo hayo kama hatoyahitaji kwenye wikiHow kwa kubofya "hide ads" upande wa kulia wa makala yoyote au kwa kufungua akaunti ya kujiunga na jamii yetu ya wahariri.


Unataka kujifunza zaidi? Fanya Matembezi ya kuifahamu wikiHow.

EditWasiliana nasi

General Questions and Help
Snail Mail

wikiHow
530 Lytton Avenue, 2nd Floor
Palo Alto, CA 94301

Press Inquiries
Community Liaison

EditMaelezo ya masharti

  1. Watu hawa wanaungana katika kuanzisha ulimwengu tunaoutaka.

Article Info

Categories: WikiHow Language Projects

In other languages:

العربية: عن ويكي هاو, Français: À propos de wikiHow, Nederlands: Over wikiHow, Português: Sobre o wikiHow, Español: Acerca de wikiHow

Thanks to all authors for creating a page that has been read 4 times.